CGI DKT. ANNA MAKAKALA AMPONGEZA RC MNDEME
Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Jeshi la Uhamiaji Tanzania CGI. Dkt. Anna Makakala amempongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwa namna ambavyo anafanya kazi za kuwahudumia wananchi pamoja na namna ambavyo anashirikiana na Jeshi la Uhamiaji sanjari na Vyomho vingine vya Ulinzi na Usalama jambo ambalo linaifanya Shinyanga kuwa salama wakati wote.
Hayo yamesemwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wakati CGI Dkt. Anna alipofika kwa ajili ya kusalimiana na kusaini kitabu cha wageni ambapo pamoja na mambo mengine lakini pia alimuahidi Mhe. Christina Mndeme kuwa ataongeza nguvu zaidi Mkoani hapo mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya askari yanayoendelea hivi sasa ili kuimarisha zaidi eneo hilo.
"Nikupongeze sana Mhe. Mndeme kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi na kuimarisha ulinzi na usalama hapa Shinyanga jambo ambalo linawafanya wananchi waemdelee kuchapa kazi za kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla, na pia nikuahidi kuwa nitaongeza nguvu hapa ili kuimarisha kazi za Uhamiaji hapa Shinyanga," alisema CGI Dkt. Anna.
Katika ziara hii CGI Dkt. Anna ameambatana na Afisa Uhamiaji Makao Makuu Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji (AC) Elizabeth Lukuwi, Mkuu wa Kitengo cha Majengo Uhamiaji Makao Makuu Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji (AC) Martine Mwenda na Mkaguzi wa Uhamiaji Said Kassim kutoka Kitengo cha Mipango Uhamiaji Makao Makuu.
PICHA NA MATUKIO
Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa suluali ya bluu) akiwa na CGI Dkt. Anna Makakala wakifurahia jambo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa