Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Venant Mboneko mapema leo tarehe 06/08/2018, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mhe. Mboneko ameanza kazi yake rasmi kama Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akichukua nafasi ya Bi. Josephine Matiro, kutokana na mabadiliko ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Makatibu Wakuu yaliyofanywa na Mhe. Rais John Pombe Magufuli mnamo tarehe 28/07/2018.
Akizungumza na viongozi mbalimbali na watendaji waliohudhuria hafla hiyo, Mhe. Mboneko amesema anamshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuwatumikia wananchi wa Shinyanga.
Amewaomba viongozi pamoja na wananchi kumpa ushirikiano kwani hawezi kufanya Shinyanga iendelee bila ushirikiano wao. " Nimekuja Shinyanga kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi, lakini siwezi kufanya peke yangu bila ushirikiano na viongozi wenzangu, watumishi na wananchi" amesema Mboneko.
Mhe. Mboneko ambaye ni Mkuu wa Wilaya wa 20 tangu kuanzishwa kwa Wilaya hiyo, ameahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Shinyanga na kuwahakikishia wananchi Ulinzi na Usalama unaendelea kuimarika.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa