Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga ambaye pia ni mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 17 Januari, 2025 amekutana na Tume ya Rais ya Kukusanya Maoni ya Maboresho ya Kodi iliyofika Ofisini kwa lengo la kujitambuisha na kufanya mazungumzo mbalimbali huku akiwakaribisha wajumbe hao mkoani Shinyanga.
Tume hiyo ambayo hapa Shinyanga imeongozwa na CPA. Leonard Mususa ambaye amemwakilisha Mwenyekiti wa Bodi Balozi. Ombeni Sefue imekuja na lengo la kupokea maoni ya wadau wa kodi ili kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa mapato nchini kwa njia shirikishi na isiyokuwa na malalamiko.
Kupitia maoni yanayokusanywa, serikali inalenga kuboresha mazingira ya ulipaji kodi, kukuza uchumi, na kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa kiwango bora zaidi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa