Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Taraba amekemea tabia ya baadhi ya Waganga wa Kienyeji Mkoani hapa ya kuwapa dawa mabinti wadogo kwa madai ya kuwaosha ili waolewe.
Mhe. Taraba akizungumza na wananchi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani tarehe 1 Desemba, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Kishapu, kata ya Ukenyenge, kijiji cha Negezi amesema tabia hiyo inayotokana na mila potofu inachochea ndoa, mimba za utotoni na hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.
"Ugonjwa wa UKIMWI bado upo na bado hauna chanjo wala tiba isipokuwa dawa za kufubaza virusi" amesema Mhe. Taraba.
Amewataka wananchi kuendelea kujikinga na ugonjwa huo kwa kuwahimiza kupima Afya zao kila mara, hasa wanaume na kupingana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Aidha, Taraba amewakumbusha wananchi kutowanyanyapaa watu wenye Virusi vya UKIMWI na kuwa na hofu ya Mungu akisisitiza kuwa, ugonjwa huu unatokana pia na watu kutotenda matendo mema.
Maadhimisho hayo yamepambwa kwa burudani mbalimbali za ngoma za asili, mashairi na maigizo yaliyolenga kuwakumbusha wananchi kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI.
Angalia Matukio mbalimbali ya maadhimisho hayo katika picha hapa chini
Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Mkoani Shinyanga, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Taraba, akiingia uwanja wa Shule ya Sekondari Ukenyenge yalipofanyika maadhimisho hayo Kimkoa hapo tarehe 01 Desemba, 2019
Diwani wa Kata ya Ukenyenge akimkaribisha Mgeni Rasmi na wananchi wote katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika kata hiyo
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ukenyenge Wilaya ya Kishapu wakifuatilia matukio katika uwanja wa shule hiyo yalipofanyika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Kimkoa
Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Shinyanga Dkt. Mlacha, akitoa taarifa ya hali ya maambukizi katika Mkoa
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Bw. Joachim Otaru, akimkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza na wananchi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya Dkt. Rashid Mfaume akitoa ujumbe wa siku ya UKIKWI Duniani mwaka 2019
Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo wakifuatilia matukio yanayoendelea uwanjani hapo
Mgeni rasmi akipata maelezo katika banda la wadau wa masuala ya UKIMWI kuhusu faida na matumizi ya Kondomu kama kinga ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa