Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamingi Macha amewashauri wananchi kutopapa shida ya kusafiri nje ya Mkoa wetu kwenda Mwanza, Dar es salaam au mkoa mwingine wowote kwa ajili ya kufuata huduma za kitibabu kwani kwa sasa zinapatikana hapa hapa Shinyanga huku akitolea mfano wa uwepo wa daktari bingwa kabisa wa pua, masikio na kinywa katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala - Kahama.
RC Macha ameyasema haya tarehe 27 Julai, 2024 alipokuwa akifunga maonesho ya Afya Code Clinic iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kupitia Idara ya Afya kwa kushirikiana na Jambo Group kupitia Jambo FM ambapo pamoja na mambo mengine lakini wananchi wamewezapata huduma ya vipimo, elimu na tiba bure bila malipo kutoka kwa wataalam na watoa huduma mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, The Agakhan Hospital, Chuo cha Afya Kolandoto nk.
"Niwashauri wananchi wote wa mkoa wa shinyanga na maeneo jirani kuwa, sisi Shinyanga kwa sasa tunao madaktari bingwa wengi ambao hapo awali wananchi mngeweza kusafiri kufuata huduma hizi Mwanza, Dar es Salaam au mkoa mwingine mbali lakini hivi sasa wapo hapa hapa Shinyanga ni jambo la kumpongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hasaan kwa kuwezesha upatikanaji wa wataalam hawa, vifaa tiba na dawa pia," amesema RC Macha.
Kando na hili, pia amesisitiza sana kuendelea na kuongeza kwa wataalamu wa afya zaidi katika utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga dhidi ya magonjwa kuliko kutanguliza tiba huku akitoa wito kwa wananchi wa mkoani Shinyanga kujiwekea utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara pamoja na kupata matibabu mapema.
Kwa upande wake Meneja wa Jambo FM ndg. Nivkson George mesema kwamba walipopata wazo la kuanzisha Afya Code Clinic ndiyo wakaona watutafute wadau wa kushirikiana nao, na hapo wakakutana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wanakuwa na maisha mazuri na wenye afya njema ambapo inatajwa kuwa ndani ya siku nne za Afya Vode Clinic wananchi zaidi ya elfu 7 wamepata huduma mbalimbali za afya bure.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa