Na. Paul Kasembo, KISHAPU DC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu isilewe na kujisahau baada ya kupata Hati Safi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na badala yake iwatie moyo wa kuongeza juhudi, maarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ili waendelee kuipata Hati Safi kila ukaguzi unapofanyika, huku akisisitiza kuongeza umakini na kuzingatia taratibu za kihasibu na wafanye vizuri zaidi.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 24 Juni, 2024 wakati akichangia hoja kwenye Mkutano wa Baraza Maalum la Madiwani linalojadili maagizo ya CAG ambapo pia ametumia nafasi hii kuitaka Halmashauri kuongeza umakini na kuzingatia zaidi taratibu za kihasibu ambazo ndiyo mwishoni hutoa hatma ya kupata Hati Safi au vinginevyo.
"Pamoja na kuwapongeza kwa kupata Hati Safi ya CAG, lakini niwaombe msilewe na badala yake sasa muongeze juhudi na muongeze umakini zaidi katika utekelezaji wa majukumu yenu namzingatie taratibu zote za kihasibu ili muendelee kupata hati safi kila ukaguzi unapofanyika,"amesema RC Macha.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amezitaka Halmashauri zote sita (6) zinazounda Mkoa wa Shinyanga kuanza kutenga fedha kutoka vyanzo vyao vya mapato ili kuweza kulipa deni la litokanalo na mkopo wa Mradi wa Upimaji Viwanja vya kuuza ambapo Halmashauri zilikopa kwa lengo la kupima na kuuza ikiwa ni sehemu ya kuongeza pato deni ambalo hivi sasa linajitokeza sana kwenye hoja za CAG.
Akiwasilisha taatifa ya Utekelezaji wa Maagizo ya CAG ambaye ni Mweka Hazina ndg. George Sumbwe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu ndg. Emmanuel Johnson amesema kuwa katika Kishapu ilikuwa na Hoja 48 ikijumlisha na hoja za nyuma ambapo 10 zimefungwa, 36 zipo hatua mbalimbali za utekelezaji, 1 imepitwa na wakati huku 1 haijatekelezwa.
Kwa upande wake CPA Yusuph Mabwe ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa nje wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Shinyanga amesema kuwa maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na wajumbe wameyachukua na watafanyia kazi.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa