RC MACHA AIPONGEZA SHINYANGA MC KUIBUKA KIDEDEA KATI YA MANISPAA ZOTE 19 NCHINI KWA USAFI
Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira yaliyohusisha Manispaa 19 Nchini huku akiwataka watumishi kuongeza kasi ya kuchapa kazi katika sekta zote ili kuweza kuyaisha na kutafisiri maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwatumikia Watanzania na kuwaletea maendeleo.
Pongezi hizi zimetolewa leo tarehe 16 Mei, 2024 na RC Macha alipokutana na Watumishi wa Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kutambuana na kukumbusha wajibu na majukumu ya kila mtumishi katika eneo lake la kazi ambapo pamoja na maelekezo mengine lakini pia amewataka watumishi kupendana, kushirikiana, kuwa wazalendo na kuyokubali kugawanywa kwa namna yoyote.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro (Wakili) amemshukuru sana RC Macha kwa pongezi hizo za ushindi, lakini pia amempongeza kwa kazi nzuri anazozifanya katika kuwatumikia Wanshinyanga huku akimuahidi kuwa yale yote aliyoelekeza wanakwenda kuyatekeleza kwa weledi mkubwa na kuleta tija zaidi kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga
Katika mashindano hayo, Manispaa.ya Shinyanga imeshinda na kuwa ya kwanza Kitaifa kwa kupata asilimia 95 ya alama zote zilizowekwa na Wizara ya Afya ikifuatiwa na Manispaa ya Moshi ambayo imepata asilimia 87 wakati nafasi ya tatu imechukuliwa na Manispaa ya Iringa ambayo imepata asilimia 83.
RC Macha anaendelea na ziara zake katika Halmashauri zote 6 zinazounda Mkoa wa Shinyanga ambapo kesho ni zamu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo kuko pamoja na mambo mengine atakagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na baadae atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Iselamagazi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa