Na. Paul Kasembo - Msalala, Kahama.
MKUU wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita ameendelea na ziara yake ya kupokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi maeneo mbalimbali ya Wilaya bila kujali vikwazo anavyokutana navyo kama vile mvua kubwa inayopelekea kuharibika kwa miundombinu ya barabara, hku akisisitiza kuwa "Iwe mvua, iwe jua lazima kuwafikia wananchi walipo na kutatuankero zao".
Aidha, Mhe Mboni amesema kuwa, katika kuendelea kutafsiri maono ya Mhe. Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni muhimu zaidi kuwapa kipaumbele wananchi, maslahi yao ili kuwaletea maendeleo ya kweli.
Katika utekelezaji wa zoezi hili, Mhe. Mboni amepokea kero zinazowakumba wamiliki wa Kampuni za uchimbaji wa madini nankuzipatia ufumbuzi na baadhi ya kero amemuelekeza Afisa Madini Mkazi (RMO) kufanya kikao na wadau wote wanaojihusisha na uchimbaji wa madini na kujadili changamoto hizo kwa pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha meendelea kuwaelekeza na kuwasizitiza Wadau wa uchimbaji wa madini kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayozunguka migodi yao na kuzingatia kuwa, jamii inanufaika ikiwa ni pamoja na ajira ndogondogo (casual labour) ndani ya migodi yao.
Kando na hayo, DC Mnoni, amewaelekeza wadau wa uchimbaji wa madini kuzingatia utunzaji wa mazingira na kuwa na Mpango Mkakati wa muda mrefu wa Utunzaji wa Mazingira (Environmental Management Plan) na kuzikumbusha Kampuni za uchimbaji wa madini kuimarisha kushirikiana na Halmashauri pamoja na Jamii katika kutekeleza Miradi ya CSR ili kutekeleza miradi ya vipaumbele na kuwa na miradi inayotokana na sauti za wananchi.
Mwisho DC Mnoni amemwelekeza Mkurugenzi wa Kampuni ya uchimbaji ya SOJEM kulipa kodi ya Serikali anayodaiwa ya Dollar 3,500 ambapo Mkurugenzi huyu ameahidi kulipa ndani ya siku 14 zijazo kuanzia sasa.
MATUKIO KATIKA PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa