Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, kuhakikisha wanatumia mfumo wa kielekroniki katika ukusanyaji wa mapato kwenye maeneo yote ili kudhibiti upotevu wa mapato.
Mhe. Jafo ametoa agizo hilo mapema leo tarehe 14 Mei, 2018 alipotembelea Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kukagua ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Shinyanga zinazojengwa chini wa ufadhili wa Benki ya Dunia.
" Hatutarajii tuendelee kutumia vitabu ambavyo wengine wanachapisha, wanakusanya mapato ya Serikali lakini mapato yanaingia kwenye mifumo isiyo sahihi" amesema Mhe. Jafo.
Jafo amewaelekeza Maafisa TEHAMA wa Mikoa na Halmashauri, kuhakikisha maeneo yote yanafungwa na yanatumia mfumo wa kilelektroniki na kuwa, katika vituo vya Afya vinavyojengwa lazima visimikwe mfumo wa kielektroniki pale tu vitakapokamilika.
Aidha, Mhe. Jafo amesisitiza katika suala la usimamizi wa miradi ya maendeleo na kuwataka Wakurugenzi wote kutopata hati chafu ikiwemo kujibu hoja zote za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Amewataka pia kutumia kutumia vizuri fedha za ujenzi wa Vituo vya Afya zilizotolewa na Serikali hususani kwa kutumia mafundi waliopo ndani jamii husika (local fundi).
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa