CHAMA Cha Ushirika Kahama (KACU) kimetoa hundi ya malipo ya pamba awamu ya pili ikiwa ni sehemu ya malipo yatokanayo na faida waliyoizalisha kwa msimu wa kilimo uliopita, huku wakianisha baadhi ya malengo yao ikiwemo kuanzisha ujenzi wa mtambo wa kukamua mafuta na kutengeneza mkaa ifikapo Machi, 2024 ikiwa pia ni utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Christina Mndeme, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Akitoa taarifa ya awali kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya KACU LTD Ndg. Tano Mwandu alisema kuwa, KACU inakwenda vizuri sana ambapo kwa msimu wa kilimo 2023/2024 wamefanikiwa kununua jumla ya kilo za pamba mbegu 5, 175, 466 zenye zaidi thamani ya Tzs. Bilioni 5.4 kutoka kwa Halmashauri 4 za Ushetu, Msalala, Kahama Manispaa na Kishapu ambazo ni sawa sawa na 86.26% ya lengo la kununua kilo Milioni 6.
Pamoja na kumpongeza Mrajis Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace kwa kazi nzuri anazofanya, pia RC MNDEME ameipongeza sana Bodi yote, wadau ikiwemo Benki ya Wakulima TADB, wakulima na watumishi wote kwa ujumla wao kwa kazi bora kabisa wanazozifanya jambo ambalo leo limetoa matunda yenye tija kwa pande zote na wote wameona.
"Nawapongeza sana Bodi ya KACU LTD, Mrajis Msaidizi wa Mkoa, watumishi, wadau ikiwemo na TADB BANK na watumishi kwa kazi nzuri mnayoifanya ambayo leo tunashuhudia mafaniko ya wazi kabisa, nyote mnastahili pongezi za dhati kabisa katika hili, sasa ongezeni kasi ili mfikie malengo kwa mwaka huu kama mlivyojipangia", amesema RC MNDEME.
Aidha RC MNDEME alipongeza sana Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita na Mbunge wa Jimho la Ushetu Mhe. Emmanuel Charahani @cherehanipeter kwa kazi nzuri wanazozifanya za kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.
Pamoja na mambo mengine kwa mwaka huu KACU LTD inatarajia kuanza kutekeleza mradi wa kukamua na kusafisha mafuta, kutengeneza mkaa ili kupngeza mnyororo wa thamani wa zao la pamba na hatimaye kuongeza faida itokanayo na mradi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa