Na. Shinyanga RS.
Kamati ya maandalizi ya tamasha la utamaduni wa msukuma Shinyanga yaani SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL imefika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme kwa lengo la kujitambulisha .
Hili ni Tamasha ambalo lilianza rasmi mwaka 2022 chini ya kampuni ya The BSL INVESTMENTS COMPANY LIMITED ambao wadau na waandalizi wakuu wa Tamasha hili.
Lengo kuu ni kuendeleza na kukuza utamaduni wa msukuma pia kutoa fursa mbalimbali kwa wasanii wa asili kukuza na kuendeleza vipaji vyao, kutoa fursa kwa wafanyabishara kuuza na kutangaza biashara zao sambamba na kufanya harambee ya kuchangia ujenzi wa shule shikizi Nhelegani iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Akitoa salamu za Kamati Ndg. Peter Black alisema kuwa, kwa ujumla maandalizi ya mwisho yamekamilika kuelekea siku ya tamasha hili tarehe 8 &9/7/2023 katika viwanja vya shule ya msingi Nhelegani huku akiwakaribisha Wananchi wote kwenye tukio hilo.
Kwa upande wake Mhe. Mndeme aliwakaribisha sana Kamati, akaipongeza kwa kuja wazo hilo lakini pia aliwahakikishia ushirikiano wakati wote kabla, wakati na hata baada ya Tamasha.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa