Na. Shinyanga RS.
KAMATI ya Siasa Mkoa wa Shinyanga imeanza ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo kwa leo tarehe 19 Februari, 2024 Kamati imekagua miradi mitatu katika Halmshauri ya Msalala ikiwemo ujenzi wa stendi ya mabasi iliyopo Isaka, jengo la utawala na Kituo cha Afya Segese na kupongeza sana utekelezaji wa mradi jengo la utawala huku likitajwa kuleta tija na ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Ndg. Mabala Mlolwa ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa Halmashauri zote 6 za Mkoa.
Akizungumza baada ya ziara hii Mhe. Mboni Mhita DC Kahama ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema kuwa, anaishukuru sana Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga kwa kufika na kukagua utekelezaji huu wa Ilani ya CCCM kwani kwa kufanya hivi kunasaidia sana kuona kama wapo katika njia sahihi au warekebishe.
"Ndugu Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga, nichukue fursa hii kuwapongeza kwa kufika na kukagua miradi yetu hii ya kimkakati, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga nipende kusema tu kuwa yote mliyoshauri na kuelekeza tumeyapokea na tunawaahidi kwenda kuyatekeleza kwa weledi na ufanisi mkubwa zaidi", amesema Mhe. Mboni.
Aidha Mhe. Mboni pia amemshukuru san Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha nyingi za miradi ya mendeleo ambapo kupitia Sekta mbalimbali wanaendelea kutekeleza ikiwemo miradi ya kimkakati ya Stendi mpya ya Isaka ambayo itakuwa pia ni sehemu ya chanzo cha mapato ya Halmashauri.
Kamati pia imetembelea na kukagua miradi ya jengo la utawala ambalo limeongeza ari, tija na utawala bora katika utoaji wa huduma kwa wananchi wa Msalala na ujenzi wa Kituo cha Afya Segese ambapo kukamilika kwake kunakwenda kuondoa adha ya wananchi kufuata huduma ya Kituo umbali mrefu na hapo awali ilikuwa stendi mpya ya Isaka.
Hii ni Halmashauri ya kwanza kati ya 6 zitakazoqngaziwa na Kamati hii ya Siasa Mkoa wa Shinyanga, ambapo tarehe 20 Februari Kamati itakuwa Ushetu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa