Na. Shinyanga RS.
KAMATI ya Siasa Mkoa wa Shinyanga ikiongozwa na Ndugu Mabala Mlolwa imeipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Nyahanga ambayo imeanzankuyumika rasmi Januari, 2024 na kupokea wanafunzi zaidi ya 600 kutoka maeneo mbalimbali ya Manispaa.
Pongezi hizi zimetolewa leo tarehe 21 Februari, 2024 wakati Kamati ilipotembelea na kukagua ujenzi huu ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020/2025 katika Manispaa ya Kahama ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa Sekta ya Elimu (Sekondari ya Nyahanga), Afya (Zahanati ya Bukooba) na Miundombinu ( KM 1.39).
"Kwa niaba ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Shinyanga, tunawapongeza Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa kutekeleza vema Ilani ya CCM kwa vitendo, na haya ndiyo matarajio ya Chama Cha Mapinduzi kwa wananchi wake ya kuwaletea maendeleo yenye tija", amesema Ndg. Mabala.
Ndg. Mabala ameziagiza Halmashauri zote Mkoa wa Shinyanga juu ya suala la utayari kwa wananchi kuanza kuchangia chakula mashuleni ili kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa tija, jambo ambalo litapelekea kuondoa utoro na kuuongeza ufaulu pia huku akisisitiza kuwa shule ikikwama kabisa itoe huduma ya uji kwa wanafunzi.
Kamati ya Siasa, pamoja na ukaguzi wa kuona namna inavyotekelezwa Ilani ya CCM lakini piq imefanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Nyahanga ambapo imepokea, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Tarehe 22 Februari, 2024 Kamati ya Siasa itakagua utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.Sehemu ya picha ikionesha baadhi ya majengo ya Nyahanga Sekondari
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndg. Mabala Mlolwa (kushoto) akiwa na Prof. Siza Tumbo ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika ziara Wilayani Kahama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa