Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme leo tarehe 25 Septemba, 2023 amekagua kuweka Jiwe la Msingi ujenzi wa Jengo la Dhurla (EMD) litakalogharimu zaidi ya Milioni 350 katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyannga pamoja na kuridhishwa na kazi inayotekelezwa hapo lakini pia ameagiza kukamilisha ujenzi huu ifikapo Septemba 30, 2023 ili wananchi waanze kupata huduma hapa.
Mhe. Mndeme pia amekagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa madarasa 11, mabweni 4 na matundu ya vyoo 16 wenye thamani ya Milioni 860 katika Sekondari ya Old Shinyanga huku akiwaagiza kuongeza kasi ya ujenzi ili ifikapo Oktoba1, 2023 mradi uwe umekamilika tayati kwa kutumiwa huku akiwapongeza kwa ubunifu wao mkubwa ambao wameuonesha katika utekelezaji huu wa mradi ambapo kwa fedha hizo hizo ambazo zingejenga bweni la wanafunzi 80, sasa zinajenga bweni la wanafunzi 120.
Katika ziara hii pia ametembelea, kukagua na kufungua rasmi Zahanati ya Seseko katika Kata ya Mwamalili iliyogharimu zaidi ya Milioni 95 ambapo inakadiriwa zaidi ya wakazi 2700 wayanufaika na uwepo wa Zahanati hii ikiwa na lenho kuu la kuwasogezea huduma karibu amnapo itapunguza vigo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga kwa Kijiji hiki na maeneo jirani.
"Leo nimetembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi katika jengo la Dharula linalojengwa katika Hospitali yenu, ujenzi wa madarasa, mabweni na matundu ya vyoo katika Shule ya Sekondari Old Shinyanga, kufungua rasmi Zahanati ya Seseko, hakika niwapongeze sana kwa kqzi nzuri mnazofanya lakini niwatake kukamilisha miradi yote hii haraka ili ianze kutumika ili walengwa waanze kunufaika na ndiyo lengo la Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wa Shinyanga," alisema Mhe. Mndeme.
Mhe. Mndeme amehitimisha ziara hii kwa kufanya mkutano wa hadhara ambapo amesikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi huku kero kubwa ikijirudia ya ukosefu wa nishati ya umeme na kuchakaa kwa miundombinu iliyopo ya maji. Ambapo Mhe. Mndeme alimtaka mkandarasi wa REA kuhakikisha anafikisha umeme eneo hilo ifikapo Oktoba 30, 2023 na kwa upande wa maji SHUWASA wameahidi kurekebisha kasoro hizo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa