DODOMA.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni leo tarehe 9 Septemba, 2024 ameshiriki Mkuatano wa Wadau wa Mazingira kuhusu Mwelekeo wa Mazingira nchini.
Katika Mkutano huu ambapo Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango umejadili mambo mbalimbali huku Mhe. Mpango akitoa wito kwa washiriki wa Mkutano huu Maalum wa Mazingira kuainisha namna bora ya kufikia matokeo tarajiwa kwa kutafuta majibu ya changamoto za kimazingira zilizopo nchini kususani katika changamoto ya uimarishaji wa mfumo wa usimamizi wa mazingira.
Mkutano huu unafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mkoani Dodoma ambapo Mhe. Mpango amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu ya Biashara ya Kaboni ambayo ni fursa katika kukabiliana na uharibilifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa