ISAGEHE - KAHAMA.
WAZIRI wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameiagiza Tume ya Umwagiliaji (NIRC) kuhakikisha mradi wa bwawa la umwagiliaji lililopo kijiji cha Malenge, Kata ya Isagehe wilayani Kahama lenye ukubwa wa mita za ujazo 600,000 na thamani ya Bil. 2.5 linajengwa unasajiliwa kwa jina la SHIJA badala ya jina la awali la MALENGE.
Bashe ameyasema haya katika ziara yake wilayaninKahama ambapo pamoja na mambo mengine lakini pia amekagua mradi huu unaojengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali na ufadhili wa Mgodi wa Barrick huku akimshukuru sana mzee Shija Lukinga ambaye awali alikuwa mmiliki wa eneo hilo na baadae kulitoa bure ili kupisha utekelezwaji wa mradi huu ambao unatajwa kuwa na tija zaidi kwa wakulima na wanamchi wa maeneo haya.
"Hii ni taswira na kipaji cha kipekee kabisa alichonacho mzee Shija cha kujitoa na kujitolea eneo lake ili kujengwa bwawa ambalo litawanufaisha wakulima takribani 427 na kuanzia sasa mradi huu usajiliwe kwa jina la SHIJA badala ya MALENGE kama ilivyokuwa ikisomeka awali," amesema Mhe. Bashe.
Aidha ameagiza kusakafiwa kwa mifereji yenye urefu wa kilometa 12 na kujenga hekta 400 za tuta zilizobakia na kwamba wataalam wa ndani watumike katika kazi hizi za ujenzi wa bwawa, ghala na kinu.
Kando na hayo pia Bashe amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kufanya kikao vha ujirani mwema na Mkuu wa Mkoa wa Tabora ili Bonde la Manonga liweze kulindwa kwa ajili ya miundombinu ya uzalishaji wa chakula badala ya kujenga nyumba za makazi.
Kukamilika kwa usanifu uliolekezwa na Mhe. Bashe utawawezesha wakuli takribani 427 kunufaika na kilimo cha uhakika ambapo sasa wataweza kuvuna hadi mara tatu kwa mwaka.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa