Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Lyamidati katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mapema leo tarehe 21/08/2019, Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, amezitaka Halmashauri nchini kuhakikisha zinakamilisha maboma yanayoanzishwa na wananchi ikiwemo shule ili kuwapunguzia umbali wanafunzi.
Mhe. Balozi akiwa kijijini hapo amekagua madarasa yaliyojengwa kwa fedha za mpango wa kuboresha Elimu (Equip – T) kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaoanza darasa la kwanza kutotembea umbali wa kilometa 5 kufuata shule ya msingi, ambapo wananchi wa kijiji hicho wameamua kuchangia na kuongezea vyumba vinne vya madarasa na ofisi moja ili kujenga shule kamili.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa madarasa hayo, Afisa Mtendaji wa kijiji Bw. Deus Maina, amesema kuwa gharama iliyotumika kutokana na nguvu ya wananchi, Serikali ya kijiji na mfuko wa Jimbo ni sh. 5,740,000. Aidha, fedha iliyotolewa na Equip –T ni sh. 6,600,000 pamoja na mfuko wa lipa kulingana na matokeo unaoitwa EP4R sh.12,500,000.
Katika taarifa hiyo, Afisa Mtendaji amesema fedha inayotakiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi ili shule iweze kusajiliwa ni sh. Milioni 25.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Hoja Mahiba kuangalia uwezekano wa kukamilisha shule hiyo kutokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa