Na. Shinyanga RS.
KAIMU Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyinga Mhandisi Samuel Joel Mwambungu amesema kuwa, ndani ya kipindi cha uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, TANROADS Shinyanga imepokea kiasi cha zaidi yaTzs. Bilioni 325 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya miundombinu ya barabara, madaraja na Uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Haya yamebainishwa leo tarehe 9 Machi, 2024 na Mha. Joel alipokuwa akizungumza na wanahabari kuwaelezea Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita ndani ya kipindi cha miaka mitatu ambapo pamoja na kueleza mazuri mengi ambayo Mhe. Rais ameifanyia TANROADS Shinyanga lakini pia Mha. Joel amemshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa anayowafanyia wanashinyanga katika kuwaboreshea miundombinu ya barabara.
"Namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi na juhudi nzuri na kubwa ya kuwaletea maendeleo wanashinyanga hasa katika miundombinu ya barabara, madaraja na ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Shinyanga ambapo ndani ya miaka mitatu ya uongozi wake mahiri TANROADS Shinyanga imepokea zaidi ya Tzs. Bilioni 325," amesema Mha. Joel.
Pamoja na mafanikio haya Mha. Joel amemshukuru pia Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha kiasi cha Tzs. Bil. 47.2 zilizoelekezwa kwa Wakandarasi Wazawa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera yake kupitia Wizara ya Ujenzi kuhusu Local Content Strategy.
TANROADS Shinyanga unahudumia Mtandao wa Barabara wenye jumla ya Km 1, 177.74 na jumla ya Madaraja 309 (kilomita 277.10 ni barabara kuu, kilomita 787.54 ni barabara za Mkoa wakati kilomita 113. 1 barabara zilizokasimiwa)
Aidha Mha. Joel amewataka wananchi kuacha kufanya ahughuli za kibinadamu pembezoni mwa hifadhi ya barabara na badala yake waitunze sanjari na kuacha hujuma dhidi ya miundombinu ya barabara ikiwemo na alama zake.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa