#shinyanga_rs
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa uwepo wa Mafunzo ya Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio nje ya Shule - IPOSA ni mkombozi kwa vijana walio wengi ambao wanaokosa fursa ya elimu ya kawaida, kwani inawezesha kupata stadi za maisha, ujasiliamali, na ufundi wa awali hivyo kuwaandaa kwa ajili ya kujiajiri na kuajiriwa.
Akizungumza Mei 23, 2025 wakati wa halfa ya ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku 21 na yaliyolenga kuwajengea uwezo walimu na viongozi wa elimu mkoani Shinyanga, Mhe. Macha alilipongeza sana Shirika la Kimataifa la Korea International Agency (KOICA) kupitia Serikali ya Korea Kusini kwa kuwajengea uwezo viongozi hao ili wakatekeleze kwa ufanisi Programu hiyo muhimu.
"Kwa dhati kabisa tuseme, uwepo wa Mafunzo ya Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio nje ya Shule - IPOSA ni mkombozi kwa vijana walio wengi ambao wanaokosa fursa ya elimu ya kawaida kwani inawezesha kupata stadi za maisha, ujasiliamali, na ufundi wa awali hivyo kuwaandaa kwa ajili ya kujiajiri na kuajiriwa wao wenyewe," alisema Mhe. Macha.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa ufadhili wa KOICA kupitia Serikali ya Korea Kusini kunatajwa kuwaongezea maarifa zaidi vijana ambapo watafundishwa kusoma, kuandika, kuhesabu, mafunzo ya ufundi stadi pamoja na ujasiliamali. Lengo ni kuwasaidia kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira na kuwawezsha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii zao.
Awali Mkurugenzi wa Taasisi ya TEWW Profesa Philipo Sanga alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wake itaendelea kuboresha Sekta ya Elimu huku akisisitiza kuwa mafanikio ya awamu ya kwanza ya IPOSA yaliwavutia wadau wengi na hivyo KOICA imeamua kuendelea kufadhili awamu ya pili ya program hii na ambayo itawafikia vijana walio wengi zaidi katika Mikoa mbalinbali ikiwemo Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa