KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu Paul Makonda amemuagiza Naibu Waziri wa Ardh, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda kufika katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kwa ajili ya kutatua kero za wananchi zinazohusu migogoro ya ardhi.
Haya yamesemwa na ndugu Makonda hapa Kahama tarehe 27 Januari, 2024 katika mkutano wa hadahra uliofanyika viwanja vya Magufuli na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi ambapo pamoja na maelekezo mengine lakini pia amewaeleza wananchi namna ambavyo CCM inawajali, inawathamini na kuwatekelezea mahitaji yao kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
"Nimefika hapa Wilaya ya Kahama, na hapo nipo kwenye mkutano wa hadhara wananchi wanakusikiliza hivi sasa, nakuagiza ufika hapa Kahama mara baada ya Bunge kuisha ili utatue kero na migogoro ya ardhi hapa", alisema Makonda.
Katika hatua nyingine Makonda alifika Halmashauri ya Msalala ambapo aliwaeleza wananchi wa Kakol kuwa ujenzi wa barabara kutoka Kahama - Kakola utaanza rasmi Februari, 2024 huku akimpigia simu Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso kuhusu kuwqfikishiq huduma ya maji wananachi wa Kakola ambapo Mhe. Aweso alisema ndani ya miezi 6 maji ya Ziwa Victoria yatakuwa yamefika Kakola.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa