Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameziagiza Mamlaka na Taasisi zote zinazodaiwa na KASHWASA kulipa madeni yao yote kwa wakati na kwa muda waliokubaliana ili kuiwezesha kutoa huduma bora na stahiki kwa wananchi wa Mikoa hii sita (6) inayoihudumia huku akitoa wito pia kwa wananchi kulipa Ankara zao kwa wakati zaidi na kuepuka usumbufu pindi wanapokatiwa huduma ya maji.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 22 Mei, 2024 alipokuwa akifungua Kikao cha kupata taarifa ya Mpango Biashara wa KASHWASA kwa mwaka 2024/2025 na 2026/2027 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi ya KASHWASA na kuhudhuriwa na viongozi wa Bodi, Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji, Menejimenti ya RUWASA, Menejimenti ya KASHWASA, na Makatibu kutoka Vyombo vya Watoa Huduma za Maji Ngazi ya Jamii katika maeneo yote yanayohudumiwa na Ziwa Victoria.
"Nizielekeze Mamlaka za Maji na Taasisi zote zinazodaiwa fedha na KASHWASA kuhakikisha mnalipa madeni yote kwa wakati na kwa muda mliokubaliana ili kuwaezesha maboresho katika utoaji wa huduma na kuimarisha uzalishaji", amesema RC Macha.
Kando na wito huu, RC Macha amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kuguatilia na kufahamu kama kuna namna yoyote ile inayopelekea ongezeko la ankara/bili zao kupitia mifumo ya mabomba katika nyumba zao ili kuepuka kuzilaumu Mamlaka za Maji kuwa zinawaongezea gharama katika mara ankara zinapokuwa zimetolewa.
Aidha amezitaka Mamlaka za Maji kudhibiti na kupunguza kama siyo kuondoa kabisa changamoto ya upotevu wa maji katika uzalishaji au usambazaji ambapo kwa sasa inakadiliwa kufikia asilimia 21 kiasi ambacho amekitaja kuwa ni kikubwa sana kwa dhana ya upotevu.
Akitoa taarifa kikaoni Mkurugenzi Mtendaji wa KASHWASA Mha. Patrick Nzamba amesma kuwa uwepo wa Kikao hiki leo ni utekelezaji wa Sera ya Maji ya mwaka 2002 kwamba uendeshaji wa huduma ya maji vijijini utafanywa kwa zingatia Mpango Biashara ulioandaliwa na Mamlaka na kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kama ambavyo leo kikao kimeanza kujadili kwa miaka mitatu ijayo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa