Mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira nchini zimetakiwa kukusanya mapato na kuwekeza katika kuzalisha, kuuza maji na kuwekeza katika miradi ya maji bila kutegemea Wizara ya maji na umwagiliaji.
Waziri wa maji na umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amesema hayo mapema leo alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya ziara yake yenye lengo la kuzungumza na Mamlaka za maji Mkoani hapa.
Profesa Mbarawa amesema fedha zilizopo kwenye mfuko wa maji Wizarani ni kwa ajili ya kuwasambazia maji wananchi walio vijijini kwa hiyo Mamlaka zitumie fedha zinazopatikana kutokana na kuuza maji kujiendesha zenyewe, aidha watafute wateja na kuhakikisha hakuna upotevu wa maji.
Mbarawa pia amewataka wahandisi wa maji kuwa waadilifu hususani katika kuteua wakandarasi na kusimamia miradi mbalimbali inayotekelezwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa