MANISPAA YA SHINYANGA YA 18 KITAIFA KATIKA UTOAJI WA HABARI KWA UMMA
Na. Paul Kasembo, Dar es Salaam
HALMASHAURI ya Manispaa ya Shinyanga imeshika nafasi ya 18 katika utoaji wa taarifa kwa Umma baada ya tathimini iliyofanywa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuangalia namna Wizara, Taasisi, Sekretarieti za Mikao na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa taarifa kwa Umma kwa kipindi cha mwaka 2023/2024.
Jumla ya Halmashauri 20 zilichaguliwa kulingana na wingi wake, amba0o pamoja na mambo mengine utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita ulizingatiwa.
Utoaji wa Tuzo pamoja na Cheti cha pongezi zimetolewa leo tarehe 21 Juni, 2024 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (MB) katika kilele cha Kikao Kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali, Itifaki na Mawasiliano Serikalini kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Kipekee pongezi nyingi sana kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ndg. Alexius Kagunze kwa kuwezesha na kusaidia Kitengo cha Habari kinachotumikiwa na Afisa Habari Bi. Jesca Kipingu kufanya kazi hii kubwa na nzuri ya kuhabarisha umma ikiwa ni utekelezaji wa Takwa la Serikali la kuhakikisha wananchi wanajua nini Serikali yao pendwa inafanya katika kuwaletea maendeleo na kuwasogezea huduma karibu, pongezi pia kwa wadau wote wa habari Manispaa ya Shinyanga.
Picha ikimuonesha Afisa Habari Manispaa ya Shinyanga Bi. Jesca Kipingu akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Habari Mhe. Nape Nnauye (MB) kwa niaba ya Manispaa yake.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa