Na. Shinyanga RS.
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imepokea Tuzo na Cheti ikiwa ni pongezi kwa utekelezaji mzuri wa Mradi wa BOOST katika hafla ya Tamasha la Bibititi Mohamed lililofanyika katika viwanja vya Ujamaa Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa Pwani
Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wananchi ikiongozwa na mgeni rasmi Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa (MB) ambapo aliweza kutoa Tuzo na Cheti cha pongeza kwa Halmashauri sita (6) zilizofanya vizuri katika utekelezaji mzuri wa Mradi wa Boost na Mradi wa Sequip.
Manispaa ya Shinyanga ilipokea Mradi wa BOOST katika shule ya msingi shule Ibadakuli 'B' iliyojengwa kupitia Mradi wa BOOST kwa kujenga Madarasa ya Awali vyumba 2, vyumba vya madarasa 14, Matundu ya vyoo 22, jengo la utawala pamoja na kichomea taka kwa gharama ya Shilingi Milioni 561,100,000/= iliyopelekea Manispaa ya Shinyanga kupata Tuzo na cheti katika hafla hii.
Tuzo na Cheti vimepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa Mwl. Alexius Kagunze ikiwa ni pamoja na cheti kimoja pongezi kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ibadakuli kwa usimamizi mzuri wa mradi huu wa BOOST.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa