Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Iddi amefanya ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Shinyanga kuanzia tarehe 10 - 13 Februari, 2019 kwa lengo la kutembelea na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa.
Katika ziara yake aliyoambatana na Mkewe, Mhe. Balozi Seif ametembelea Wilaya zote tatu za Kahama, Kishapu na Shinyanga ikiwemo kuona shughuli zinazofanywa na Mgodi wa Dhahabu Mwadui, kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Kishapu ya Dkt.Jakaya Kikwete na kushiriki ujenzi wa msingi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga.
Mama Asha Suleiman Iddi, mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimpa pole mgonjwa katika wodi ya wazazi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga tarehe 12/02/2019
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Iddi akimkabidhi Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dakama, jezi jozi mbili kwa ajili ya mpira wa miguu shuleni hapo, tarehe 11/02/2019 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, o.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Iddi, akikabidhi "printer" kwa ajili ya matumizi ya kituo cha Polisi Ushetu
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Iddi akishiriki ujenzi wa msingi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga hapo tarehe 12/02/2019 katika kata ya Iselamagazi, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Waliokaa kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack na Mke wa Mhe. Balozi mama Asha Suleiman Iddi wakiwa katika mkutano na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Ushetu.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa