Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya madini kusimamia uzalishaji wa rasilimali za madini katika mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond uliopo Mwadui Mkoani Shinyanga ili kuwanufaisha Watanzania.
Mhe. Samia ametoa agizo hilo jana tarehe 28/02/2019, alipotembelea mgodi wa Mwadui katika ziara yake Mkoani hapa.
Amesema timu iliyoundwa na Wizara ya madini ifike kufanya tathmini ya mapato yanayotokana na uzalishaji wa Almasi ili mgodi huo uweze kulipa kodi inavyotakiwa kwani tangu mgodi uanze umekuwa ukishindwa kulipa baadhi ya kodi kwa madai kuwa haujapata faida.
“Pande zote inabidi tubadilike katika usimamizi, nchi ndiyo inatakiwa kunufaika na rasilimali, hatuwezi kukaa kuangalia tu wawekezaji wafanye wanavyotaka”
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa