Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ally Idd amewataka Watanzania kudumisha amani ya nchi ili kuzidi kupata maendeleo katika Nyanja zote.
Akizungumza katika Mkutano na wananchi wa kijiji cha Buganzo, kata ya Ntobo, Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 19 Agosti, 2019, Mhe. Balozi amesema amani ndiyo kila kitu katika kuboresha sekta mbalimbali.
“Wenzetu nchi nyingine wanatuonea wivu hasa katika kupokezana uongozi,siyo nchi nyingi zinafanya hivyo, hivyo ni lazima tuitunze amani yetu”
Katika hotuba yake pia, Mhe. Balozi amesisitiza uteuzi wa wagombea wenye sifa ya kuwatumikia Wananchi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Mhe. Balozi ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga, yupo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo Mkoani hapa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa