• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

Dkt. Hussein Mwinyi aridhishwa na miradi ya SUMA JKT Kanda ya Ziwa

Posted on: August 30th, 2019

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi amesema anaridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na miradi inayotekelezwa na SUMA JKT kanda ya Ziwa.

Dkt. Mwinyi akiwa kwenye ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na SUMA JKT pamoja na makampuni mengine yaliyo chini ya Wizara hiyo kanda ya Ziwa mapema leo tarehe 30/08/2019 katika Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga amesema kwa kiwango kikubwa ameridhishwa na kazi zinazofanywa na sehemu kubwa kazi zimekwenda kwa kiwango kinachotarajiwa na kuwa changamoto zilizopo zitafanyiwa kazi.

"Niwahakikishie Mikoa na Halmashauri zinazohusika na miradi inayotekelezwa na SUMA JKT changamoto zote zitafanyiwa kazi" amesema Dkt. Mwinyi.

Aidha, amemshukuru Mhe. Rais John Magufuli kwa kuiamini kampuni hiyo iliyo chini ya Wizara yake na ndiyo sababu ya yeye kufanya ziara hiyo ili kuhakikisha imani hiyo inadumu pamoja na kuwaomba viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri kuendelea kuiamini.

Aidha, amewataka SUMA JKT kuongeza kazi ya ziada mara watakapopata fedha ili kukamilisha jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambalo ujenzi wake umesimama kutokana na changamoto ya fedha.

Naye Mkurugenzi wa SUMA JKT Kanali Rajab Mabele amesema kuwa, kampuni hiyo imepiga hatua kubwa hasa katika nyanja ya ujenzi lakini pia inajihusisha na kazi nyingine mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji.

Awali, akimkaribisha Dkt. Mwinyi Mkoani hapa, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemuomba kupitia kampuni ya SUMA JKT kuangalia jinsi ya kuwa na miradi ya kuvuna maji ili wananchi waweze kujishughulisha na kilimo cha umwagiliaji.

"Pamoja na kiangazi kilichopo, tunapata mvua nyingi sana na tunavuna mpunga unaoweza kulisha nchi yote, sasa tuone namna bora ya kuvuna hayo maji na tayari baadhi ya wananchi wameshaanza kuchimba mashimo makubwa ya kuvuna maji, tumeona kama Mkoa tufanye hilo ili wananchi wetu waweze kupata mpunga" amesema Telack


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa