MHE. KATA,BI AKABIDHI MAGARI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA.
Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amekabidhi magari matatu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, huku akimpongeza Mhe. Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi na kuboresha huduma za Afya hapa nchini.
Magari yaliyokabidhiwa ni la kubebea wagonjwa (Ambulance) gari la Utawala la shughuli za usimamizi shirikishi, pamoja na gari aina ya TATA kwa ajili ya kubeba Watumishi wa afya wanapokweda kutoa huduma Hospitalini na kisha kuwarudisha majumbani mwao.
Amekabidhi Magari hayo tarehe 24 Mei, 2024 katika viwanja vya Hospitali hiyo na kuhudhuliwa na wananchi, viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama, pamoja na Wahesimiwa Madiwani.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, akizungumza katika hafla hiyo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwamba katika Utawala wake ndani ya kipindi kifupi, ameleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Afya likiwamo Jimbo la Shinyanga Mjini.
“Ninafurahi kukanidhi mqgari haya leo katika Hospitali hii ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya, na kuwajali watumishi kwa kuwapatia usafiri, tunamshukuru sana Mhe Rais Samia hapa Shinyanga katika ahadi zetu kweye Sekta ya Afya tumetekeleza zaidi ya asilimia 100 na kupitiliza kabisa, amesema Mhe. Katambi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro, amesema mambo ambayo anayafanya Katambi Jimboni kwake ni maajabu, na ni bahati ya pekee waliyonayo Wanashinyanga, kuwa na Mbunge mpenda Maendeleo na hana kelele, zaidi ya kuonyesha Vitendo.
Aidha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe.Elias Masumbuko,amesisitiza kwamba Magari hayo yatumike kwa malengo kusudiwa pamoja na kutunzwa ile yadumu kwa muda mrefu kutoa huduma.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dr. Luzila John, akisoma risala anampongeza Mhe. Rais Samia kwa namna alivyosaidia upatikanaji wa Magari hayo pamoja na Mhe Katambi, sambamba na ufuatiliaji upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya majengo ambayo hayajakamilika.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa