Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kufuata na kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya ufungaji wa hesabu za Serikali ili kuepuka kupata hoja ambazo zinaweza kupukika kirahisi.
Mhe. Mndeme amesema hayo katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ambayo ilikuwa na hoja 73 za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ikiwa hoja 30 zimeshughulikiwa na kufungwa huku hoja 43 zikiwa katika hatua mbalimbali za kutekelezwa ili zifungwe.
Kwa mujibu wa taarifa niliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Bi. Hadija M. Kabojela mbele ya mgeni rasmi na mbele ya Baraza la Madiwani na kisha kutolewa ufafanuzi wa kina na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mhe. Gagi Lala Gagi inaonesha wazi kabisa kuwa sasa Ushetu imebadilika na inakwenda kufanya vizuri sana baada ya kupata hati chafu jambo ambalo lilitoa matumaini makubwa sana ya kwamba suala la hati chafu kwa Ushetu sasa basi.
“Pamoja na maagizo haya niliyowapatia, lakini pia nawaelekeza baadhi ya mambo ya kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuendelee kujibu hoja za CAG kwa kuwa hoja 43 bado ni nyingi sana kwa Halmashauri kama ya Ushetu, muendelee kufanya usuluhishi wa mahesabu pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za ufungaji wa vitabu vya ukaguzi na katika hili nikiwakumbusha kudai madeni yote na wao kulipa madeni wanayodaiwa,”alisema Mhe. Mndeme.
Huu ni muendelezo wa vikao maalumu vinavyoendelea kwa katika Halmashauri zote ndani ya Mkoa wa Shinyanga yenye Wilaya 3 na Halmashauri 6.
Sehemu ya Waheshimiwa Madiwani wakionekana katika picha wakati wa kikao cha baraza maalumu la CAG Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
Picha ikimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (wa kwanza kushoto) akifuatilia jambo wakati wa kikao maalumu cha CAG
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa