Na.Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme ameshiriki Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambacho kilihusisha ajenda ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Baada ya kupokea taarifa na kumsikiliza (CAG) ilikabainika kuwa pamoja na kazi nzuri wanazofanya ikiwamo ya kujibu hoja lakini hawajafikisha asilimia 100 za lengo la makusanyo kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2023 hivyo akawaagiza kuhakikisha wanafikisha asilimia 100 kabla ya tarehe hiyo kwani Kishapu imefikisha 85% na Shinyanga DC ina 75% ya lengo la 100% ya mwaka 2022/2023.
“Sikubaliani kabisa na suala la kutofikishwa kwa lengo la makusanyo kwa mwaka 2022/2023, kwakuwa bado tumebakiwa na siku chache niwatake sasa kuhakikisha kuwa mnafikisha ili kuondokana na aibu ya kusomwa mbele ya Halmashauri nyingine ambazo zimefikisha. Aidha niwatake sasa muimarishe vyanzo vya mapato na kubuni vyanzo vingine sambamba na kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma ili tuweze kuwahudumia wananchi wetu,” alisema Mhe. Mndeme..
Kando na hayo, aliwapongeza sana wakurugenzi wa Halmashauri hizo, Ndg. Emmanuel Johnson wa Kishapu kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili amsaidie kazi na pia kwa kuweza kujibu hoja 22 kati ya 54, na Ndg. Simon Berege kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili amsaidie kazi katika Halmashauri ya Shinyanga na kwa kujibu hoja 90 kati ya 149 na nyingine zinazobakia zikiwa katika hatua mbalimbali za utekelezaji ili zifungwe.
Aidha aliwapongeza sana Wakuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na Mhe. Johari Samizi wa Wilaya ya Shinyanga pamoja na Waheshimiwa Wenyeviti na Madiwani wa Halmashauri hizo kwa usimamizi mzuri na ushirikiano wao wakati wote na watumishi katika kutekeleza majukumu yao na hiyo ndiyo misingi mizuri ya kuwahudumia wananchi wetu.
Picha ikionesha sehemu ya Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiwa katika kika maalumu cha CAG
Sehemu ya picha ikionesha waheshimiwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu katika kikao cha CAG
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa