Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezindua rasmi jengo kwa ajili ya makazi ya Wazee wasiojiweza leo katika Kata ya Kolandoto, Manispaa ya Shinyanga, Mkoani Shinyanga akiwa Mkoani hapa kwa ziara ya siku mbili.
Nyumba hiyo yenye vyumba 14, sebule, bustani, miundombinu ya maji na umeme imejengwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto chini ya Idara ya Maendeleo ya jamii na kusimamiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi kwa gharama ya sh. milioni 138.1, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa jiko la kisasa linalotumia nishati ya gesi.
Pamoja na mindombinu hiyo, Wazee pia wamekabidhiwa mahitaji muhimu ikiwemo masanduku ya huduma ya kwanza, vyandarua, mashuka na madawa ili kuweka mazingira salama kwa Wazee hao, ambapo pia wamewekewa Televisheni kwa ajili ya kupata habari na burudani.
Akizindua jengo hilo Mhe. Ndugulile amesema kuwa, Serikali imeendelea kufanya maboresho katika nyanja mbalimbali ikiwemo majengo ya Wazee ili kuwafanya waishi katika mazingira bora na salama kwa kutambua na kuenzi mchango wao katika maendeleo ya Taifa.
Aidha amewaagiza viongozi wote wanaosimamia makazi hayo kuhakikisha vifaa vilivyokabidhiwa kwa Wazee vinawanufaisha walengwa na siyo watu wengine huku akitoa angalizo kuwa, makazi hayo ni kwa ajili ya Wazee ambao hawajiwezi na imeshindikana kupata huduma kutoka kwa watoto wao pamoja na jamii, siyo kwa kila mzee aliyefikisha miaka
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa