RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali kwa watoto yatima wanaoishi katika Kituo cha Shinyanga Society for Orphans kilichopo Bushushu Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kuwatakia kila lenye kheri na kwamba Serikali inawajana kuwathamini.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hzio, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari M. Samizi amesema kuwa ni utaratibu wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwapatia zawadi watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu, kushiriki nao sherehe mbalimbali pamoja ambapo kwa sherehe za mwaka mpya wa 2024 Mhe. Rais ametoa zawadi kwa watoto yatima hawa wa Bushushu hapa Manispaa ya Shinyanga.
"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa 2024 kwa kutoa zawadi kwa watoto yatima 35 wa kituo hiki cha Shinyanga Society for Orphans hapa Bushushu Manispaa ya Shinyanga ambapo ametoa mchele, mafuta ya kupikia, sukari, nguo na juisi na ujumbe wake kwa watoto hawa n8 kwamba anawapenda sana, anawathamini na kuwatakia kila lenye kheri", alisema Mhe. Johari.
Kwa upande wao watoto wa kituo hiki wamemshukuru sana Mhe. Rais kwa zawadi hizi huku wakimuombea kwa Mwenyezi Mungu ili amjalie kheri, afya zaidi na mafanikio katika kuwatumikia watanzania na wasiojiweze.
Kituo cha Shinyanga Society for Orphans kilichopo Bushushu Halmashauri ya Manispaa kina watoto 35 ambapo 26 wanaosoma Shule ya Awali na Msingi na watoto 6 wanasoma Sekondari.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa