• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

MICHEZO YA JADI NI AJIRA NA UTAMBULISHO WA JAMII- KYAIBAMBA

Posted on: March 24th, 2025

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

MRATIBU wa Michezo ya Jadi Tanzania (CHAMIJATA) ndugu Abubakary Kyaibamba amesema kuwa michezo ya jadi ni ajira kama zilivyo ajira nyingine na pia ni utambulisho rasmi wa jamii flani mbele ya jamii nyingine.

Abubakary ameyasema hayo leo tarehe 24 Machi, 2025 wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati Tendaji ngazi ya Wilaya na Mkoa kikao ambacho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga huku Bi. Janeth Elias ambaye ni Afisa Utamaduni kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa akipongeza uwepo wa kikao hicho na kwamba kinakuja kurejesha uhai wa michezo hiyo.

Abubakary alisema kuwa michezo ya jadi kama ilivyowekewa msisitizo na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake inakuja na utambuzi wa jamii, kuongeza ajira, kuimarisha utamaduni na mila zetu ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga wenyeji wanautambua kama (MBINA) ni mchezo maarufu na mchezo pendwa zaidi kwa kabila la Wasukuma.

"Ndugu zangu wajumbe, michezo ya jadi ni ajira kwa vijana na utambulisho wa jamii flani mbele ya jamii nyingine kwakuwa unakuwa na tamaduni, mila na desturi zake tofauti na nyingine lakini pia inatumika kama sehemu ya ajira katika sehemu mbalimbali za burudani na michezo ambayo hukutanisha watu wengi na kuongeza mzunguko wa uchumi kwa eneo husika," alisema Abubakary.

Ujio wa CHAMIJATA mkoani Shinyanga unalenga kuchechemua, kurejesha hamasa ya mchezo huo ambapo kwa miaka ya hivi karibuni umebakiwa ukichezwa na kuadhimishwa katika sherehe za SANJO YA BUSIYA @busiyachiefdom ambayo hufanyika katika Kata ya Ukenyenge, Wilaya ya Kishapu katika viwanja vya Utemini maarufu kama BUSIYA CHIEFDOM kila ifikapo Julai ya kila mwaka.

CHAMIJATA pamoja na mambo mengine inakuja na mkakati wa kuibua vipaji zaidi kwa vijana ili waweze kuiheshimisha michezo ya jadi kama ilivyokuwa hapo awali ambapo sasa watacheza, kuenzi na kuwaunganishwa pamoja kupitia michezo hiyo jambo ambalo litaipelekea kuimarika zaidi kwa amani, upendo na mshikamano miongoni mwa jamii huku ikitajwa kuwa ni michezo ambayo haukipewa kipaumbele miaka ya hivi karibuni.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • ENDELEENI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI - DC. MBONI

    May 30, 2025
  • TAKUKURU SHINYANGA YAANZA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA UBADHIRIFU WA SHILINGI MILIONI 92 ZA WAKULIMA WA TUMBAKU WA USHETU - DONASIAN.

    May 27, 2025
  • MAISHA BAADA YA KUSTAAFU YANAHITAJI UTULIVU - DC. MTATIRO

    May 26, 2025
  • MAFUNZO YA IPOSA NI MKOMBOZI KWA VIJANA WALIO WENGI WANAOKOSA FURSA YA ELIMU YA KAWAIDA - RC. MACHA

    May 23, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa