Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya Afya na uzazi umeanza mchakato wa kuunda sheria ndogo za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa lengo la kumaliza tatizo la vifo vinavyotokana na uzazi.
Akiwasilisha mapendekezo ya sheria hizo mapema leo tarehe 03 Juni, 2019 katika kikao cha pamoja kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Msaidizi Afya Dkt. Rashid Mfaume amesema kuwa, mapendekezo hayo yatapitiwa na timu ya wataalamu wakiwemo wanasheria wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na kufuata taratibu zote za kuunda sheria ndogo ili kuhakikisha wananchi na watendaji wote wanawajibika kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Katika kikao hicho, timu ya wataalamu imeundwa ambapo baada ya wiki 3 rasimu ya kwanza ya sheria hiyo itawasilishwa kwa ajili ya kuendelea na mchakato.
Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Albert Msovela akizungumza katika kikao hicho
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya Dkt. Rashid Mfaume akiwasilisha mapendekezo ya sheria ndogo katika kikao hicho
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa