Na. Shinyanga RS.
Mkoa wa Shinyanga umefanya kikao chake cha kwanza kuelekea Uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Mama Samia ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ( MAMA SAMIA LEGAL AID NATIONAL CAMPAIGN ) utakaofanyika tarehe 12 Juni, 2023 katika viwanja vya sabasaba Manispaa ya Shinyanga..
Akizungumza wa ufunguzi wa kikao hicha cha awali Msajili ,saidizi - Wa Watoa Huduma wa Kisheria Mkoa wa Shinyanga Ndg. Tedson Ngwale ambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga aliwàambia wajumbe waliohudhuria kuwa kampeni hiyo inalenga kulinda na kukuza haki ya upatikanaji kupitia huduma za masaada wa kisheria nchini, kuimarisha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza hususani wanawake, watoto na makundi mengini yaliyo katika mazingira magumu jambo ambalo litaimarisha amani na utulivu, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na kuleta utengamano wa kitaifa.
"Ndg. Wadau wa Kampeni ya Mama Samia, nipende kuwajulisha kuwa uwepo wa Kampeni hii kutakwenda kuondoa makandokando wanayopata wananchi hasa wanawake na watoto, makundi yaliyo kwenye mazingira magumu, na wasiojiweza lakini wanahitaji kupata haki, tukifanikiwa hili hakika wananchi wote wataimarika kiuchumi, amani na utulivu utaimarika ikiwa ni pamoja na utengamano wa kitaifa pia," alisema Ngwale.
Uanzishwaji wa Kampeni hii ni utekelezaji wa Maono na azma ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha mfumo wa kutatua changamoto zinazowakumba wananchi bila kusubira wananchi hao kuwasilisha changamoto zao wakati wa ziara za viongozi wa kitaifa pamoja na uwepo wa uvunjifu wa haki za binadamu sambamba na ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake, watoto na makundi maalum.
Kampeni hii inatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu (3) 2023 hadi 2026 kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kila Mkoa, Wilaya, Kata, Mitaa na Vijiji ikiwa na kauli mbiu isemayo;
" Msaada wa Kisheria kwa Haki, Usawa, Amani, na Maendeleo".
Picha ikionesha sehemu ya wajumbe wa Kampeni wakiwa kwenye kikao cha kwanza katika Ukumbi wa Mikutano ulioo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Sehemu ya picha ikionesha wajumbe wakiwa kwenye kikao katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Picha ya muonekano wa wajumbe wa kikao wakiendelea wakati kikao cha kwanza
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa