Na. Shinyanga RS.
Mkoa wa Shinyanga umepokea rasmi na kuanza kwa Mradi wa Kuongeza Upatikanaji wa Matumizi ya
Vyakula Vilivyoongezwa Virutubishi katika Shule na jamii kwa ujumla unaosimamiwa na kutekelezwa
kwa ushirikiano baina ya Serikali na Shirika lisilo la Kiserikali la GLOBAL ALLIANCE FOR IMPROVED
NUTRITION - GAIN, pamoja na Kampuni ya SANKU Project Healthy Children Ltd.
Akizungumza wakati wa kupokea mradi huo Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Ndg. Boniphace Chambi
ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme alisema kwamba, Lishe ni
suala mtambuka sana.
Utapiamlo katika jamii ni matokeo ya mkusanyiko wa matatizo mengi sana ambayo yaweza
kusababishwa na Ulaji duni na mtindo wa maisha usiofaa, maradhi mbalimbali, kutokuwa na uhakika wa
chakula, matunzo duni ya mama na mtoto, mazingira machafu, rasilimali haba na mgawanyo wa
rasilimali usiokuwa na uwiano sahihi kijinsia, umasikini wa kipato, machafuko ya kisiasa na hata sera
zisizitambua umuhimu wa loshe kwa maendeleo ya mwanadamu na Taifa kqa ujumla.
"Ukifuatilia maelezo yangu hapo awali na ukatazma takwimu za afya kitaifa za hivi karibuni ambazo
zimebaini kuwa Mkoa wa Shinyanga unaasilimia 27.5 ya watoto walio Dumaa, na ndiyo sababu
kubwa ya kuwatafuta wenzetu GAIN na SANKU ilii kwa pamoja tuweze kushirikiana katika kutatua
mpja ya visababishi na kiwanho hiki cha udumavu katika Mkoa wetu ambapo itasaidia kupatikana
chakula kilichoongezwa virutubisho ambavyo ni Iron kwa ajili ya damu, madini ya Zinki kwa kinga ya
mwili na j8shipa ya damu, vitamini A na Foliki Asidi kwa ajili kusaidia uumbaji wa mtoto," alisema
Chambi.
Chambi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa alitumia fulsa hiyo kuwaelekeza Wakuu wa Elimu kuwa 1.Vyakula
vyote vinavyotolewa mashuleni viwe na virutunisho tajwa, 2. Wazabuni wote kuzingatia maelekezo hayo
ya virutubisho, 3. Kamati/Bodi za shule ziteue wazabuni wenye vigezo kwa muibu wa sheria na
miongozo iliyopo, 4. Taasisi zote za Udhibiti Ubora zihakikishe usalama wa chakula na kufuatilia kwa
karibu kuepuka mafhara ambayo yaweza kutokea na kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wadau
kuendelea kuyoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa virutubisho.
Kwa pande wake Ndg. Peter Kaja muwakilishi Wizara ya Afya Idara ya Kinga àlisema kuwa wapo hapa
Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya KUKABIDHI MRADI ikiwa ni moja wapo ya afua kama Wizara na
watekelezaji ambao ni TAMISEMI kwa kushirikiana na wadau ambao ni SANKU na GAIN baada ya
uzinduzi uliofanyika Wilaya ya Kahama mwezi Aprili, 2023 na leo unakabidhiwa rasmi hapa kwa niaba ya
Mikoa 6 ya Kanda ya Ziwa ambayo inashiriki na lengo ni kunufaisha wanafunzi 120,000 ikiwa ni shuke 40
kwa kila Mkoa.
Picha ya pamoja kwa washiriki wa mradi
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa