Na. Paul Kasembo, SHY RS
MKUTANO maalum wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Shinyanga Mjini imempongeza sana Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro (Wakili) kwa uwajibikaji na utendaji kazi mzuri wa kazi katika kuitekeleza Ilani ya CCM kwa kipindi cha Januari 2024 hadi Juni, 2024 huku wakimtaka kuchukua pongezi, maoni, ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe kwa lengo la kwenda kuboresha utekelezaji wa Ilani ukizingatia ndiyo inayounda Serikali.
Pongezi hizi zimetolewa leo tarehe 20 Juni, 2024 na Katibu wa CCM (M) Shinyanga ndg. Oderia Batimayo wakati wa mkutano huu uliofanyika katika Ofisi ya CCM (W) ya Shinyanga ambapo pamoja na pomgezi kwa Mhe. Mtatiro lakini pia wamempongeza sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ndg. Alexius Kagunze pamoja na Menejimenti kwa ujumla kwa kazi nzuri wanazozifanya ikiwa ni utekelezaji wa Ilani jambo ambalo linapelekea wananchi kuendelea kuiamini Serikali kupitia Sekta mbalimbali ambazo zinawagusa wananchi wote.
"Chama kinakupongeza sana Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Komredi Julius Mtatiro kwa kazi nzuri unayoifanya katika kutekeleza Ilani ya CCM hakika unafanya kazi nzuri yenye kutukuka, pia Mkurugenzi wa Manispaa ndg. Alexius Kagunze unafanya kazi njema kwa wananchi pamoja na Menejimenti yote ya Manispaa hakika ninyi ndiyo mnatufanya sisi tuendelee kuaminiwa na wananchi kupitia utekelezaji wa Sekta zenu tunawathamini sana,"amesema Oderia.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani Mhe. Mtatiro amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha na kusogeza huduma zote kwa wananchi kupitia Sekta mbalimbali huku akisisitiza kuwa TARURA ilikuwa na miradi 10 wakati anafika na 4 kati ya hiyo ndiyo ilikuwa imetekelezwa na 6 ilikuwa bado. Lakini kwa kushirikiana na wataalam wameanza kuitekeleza miradi 6 na kwa sasa ipo hatua nzuri ya ukamilishaji.
Kwa upande wa Nishati amesema kuwa TANESCO na REA wanaendelea kusambaza nishati ili kuwafikia wananchi wote pamoja na changamoto ya ucheleweshaji wa kupeleka huduma hiyo kwa wananchi huku kwa upande wa Afya akisema wameboresha zaidi.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa