Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewaasa wananchi kuachana na mila potofu za kuamini na kutumia bidhaa za nje ya nchi kuwa ni bora.
Mhe. Telack ametoa wito huo akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya uwekezaji na viwanda katika Wilaya ya Kishapu Mkoani hapa ambapo amekutana na vijana wajasiriamali wanaotumia malighafi za ndani ya nchi kutengeneza bidhaa mbalimbali.
"Watanzania tubadilike na tuthamini vitu vyetu" amesema Telack alipowatembelea vijana sita wa kikundi cha Badimi kilichopo katika kata ya Mhunze.
Baadhi ya vijana hao ambao wanatumia ngozi kutengeneza viatu wamesema kuwa watahakikisha wanatengeneza viatu kwa ajili ya Mkoa mzima lakini changamoto kubwa ni uhaba wa malighafi na mashine.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Taraba amesema kuwa kwa mwaka wa fedha unaokuja, Halmashauri ya Kishapu imetenga kiasi cha shilingi 18 milioni kwa ajili ya kuwezesha kikundi hicho.
Aidha,katika ziara yake Mhe. Telack ameweza kuona ubunifu wa kutengeneza mashine za kukoboa nafaka pamoja na mashine ya kuwezesha kulima na kupanda unaofanywa na mwananchi Daud Nkende ambaye anasema anatafuta vijana watakaoshirikiana naye kutengeneza mashine nyingi kwa ajili ya matumizi ya wakulima.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa