Na. Shinyanga RS
Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Umma Kanda ya Magharibi Ndg. Gerald A. Mwaitebele amewaapisha kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa uongozi wa umma Dr. Yudas Ndungile ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Mkoa wa Shinyanga na Bi. Fatma Mohamed ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu hafla iliyoshuhudiwa na Prof. Siza D. Tumbo ambaye ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza leo tarehe 25 Oktoba, 2023 mara baada ya tukio hili, Mwaitebele aliwaeleza kuwa kiapo hiki walihochopata kinawataka kwenda kuwa msaada kwa wananch wanaowahudumia huku akiwakumbusha kuwa cheo ni dhamana.
Kwa upamde wake Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumho aliwataka kwenda kutanguliza uzalendo, uadilifu na kuchapa kazi zaidi katika utumishi wao kwakuwa wameapa na kuaminiwa na Serikali.
Wakitoa neno la shukurani mara baada ya kiapo viongozi hao walisema, wamepokea nasaha, ushauri na maelekezo yote waliyopewa na kwamba wanakwenda kuyaishi katika utumishi wao ndani na nje ya ofisi zao.
Gerald Mwaitebele Katibu Msaidizi OR, Sekretarieti ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo
Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga (kushoto) pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu (kulia) wakiapa
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa