MWENGE WA UHURU 2023 WAPOKELEWA USHETU
Na. Shinyanga RS.
MWENGE wa Uhuru 2023 umepokelewa Halmashauri ya Ushetu amnbapo pamoja na kuiangaza Ushetu katika utekelezaji wa kuwaletea maendeleo wananchi wake yake lakini pia umeweza kuona, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 6 yenye thamani ya Tzs. Millioni 920, umekimbizwa kilomita 99 huku kivutio kikubwa kikiwa utekelezaji wa ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi iliyogharimu Tzs. Milioni 150.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim alisema kuwa Serikali ya awamu ya 6 imetoa fedha nyingi sana ili kuhakikisha kuwa wanaishi wake wanapata mazingira bora na mazuri zaidi ya kuishi na kwamba kila kukicha na kwamba Mhe. Dkt. Samia Sukuhu Hassan anapambana kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa wananchi wake wote,
Kando na mradi huo pia Mwenge wa Uhuru 2023 umefika katika kikundi cha wajasiliamali wanawake katika Kijiji cha Mpunze (Mpunze Industry Group) ambao walipata mkopo kutoka mapato ya ndani 10% ya wanawake, vijana na watu wenye ulemeavu ambao wanaendesha shughuli za kukoboa na kusaga nafaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita aliwaeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuthamini na kuwajali sana wananchi wake ambapo sasa inawapelekea miradi mbalimbali kwa lengo la kuwaondolea kero na kuwawekea mazingira kuwa bora na rafiki kwa maisha na kukuza uchumi wao.
Mwenge wa Uhuru 2023 tarehe 1 Agosti, 2023 utakuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala ambapo ndiyo Halmashauri ya 6 na ya mwosho kwa Mkoa wa Shinyanga ambapo tarehe 2 Agosti, 2023 utakabidhiwa Mkoani Geita.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa