Na. Shinyanga RS.
MWENGE wa Uhuru 2023 umeingia ndani ya Halmashauri ya Msalala ambapo umepokelewa na Ndg. Katimba Khamis kutoka Halmashauri ya Ushetu ambapo utazindua, kuona na kuweka mawe ya msingi katika miradi 4 yenye thamani ya zaidi ya Tzs. Milioni 600 na kukimbizwa jumla ya kilomita 97.8 katika Kata 7.
Akitoa taarifa ya Msalala DC mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 MkurugenI wa Halmashauri ya Ushetu Ndg. Katimba Khamis alisema kuwa, Mwenge wa Uhuru utazindua mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji kijiji cha MAsabi Kata ya Mega na kuona mradi wa utunzaji mazingira na upandaji wa miti katika Zahanati ya Msalala.
Miradi mingine ni uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Segese ambapo kuna ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara (Laboratory), jengo la mama na mtoto (maternity ward), kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu Shule ya Msingi Segese na mradi wa mwisho ni kupna kikundi cha vijana (MAFUNSDI SOFA -KAKOLA) waliopata mkopo kutoka mapato ya ndani usiokuwa na riba wa 10% wanaojishughulisha na ufundi wa samani.
Hii ndiyo Halmashauri ya mwisho kuangaziwa miradi yake na mbio za Uhuru 2013 iliyopo Wilaya ya Kahama hapa Mkoani Shinyanga ambapo kesho tarehe 2 Agosti, 2023 Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa Mkoani Geita ukitokea hapa Halmashauri ya Msalala.
Picha ikionesha kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2023 katika mojaya gati za maji - Msalala
Mmoja wa wanufaika wa mradi wa maji - Msalala akiwa amebeba ndoo kichwani kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa