Na. Paul Kasembo, Shinyanga DC.
MWENGE wa Uhuru ukiongozwa na ndg. Godfrey Mnzava umepoingeza Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) ambalo ujenzi wake ulianza kujengwa mwaka wa fedha 2022/2023 na kukamilika mwaka 2023/2024 ulipo hapa Iselamagazi.
Hayo yamesemwa tarehe 12 Agosti, 2024 mara baada ya kukagua ujenzi huu ikiwa ni moja kati ya miradi iliyofikiwa na Mwenge wa Uhuru na kuuzindua ambapo amesema kuwa kukamilika kwa jengo hili kutaongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi jambo ambalo linatafsiri kwa vitendo maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Hongereni sana kwa utekelezaji wa mradi huu bora kabisa wenye viwango wa jengo la wagonjwa wa dharula, mradi huu unakuja kuhakikisha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Shinyanga wanapata huduma za dharura badala ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizi," amesema Mnzava.
Kwa mujibu wa taarifa ya Daktari Nuru Yunge ilisema kuwa, mpaka sasa mradi huu umekamilika na jengo limeanza kutoa huduma kwa wagonjwa, ambapo imeweza kuwahudumia wagonjwa 59 kuanzia tarehe 28/2/2024 kwa mchanguo ufuatao, magonjwa ya Maralia kali 25, upungufu wa damu mkali 16, Ajali za barabarani 6, Maumivu ya tumbo 4, shinikizo la damu 2, kiharusi 3, matatizo ya upumuaji 1, uvimbe kwenye kizazi 1, na kisukali 1.
Pia amesema wamefanikiwa kupokea vifaa vya jengo la dharura kutoka Serikali kuu ikiwemo mashine ndogo ya mionzi, mashine ya kufuatilia hali ya wagonjwa, mashine ya kushtua mapigo ya moyo, mashine ya kusaidia kupumua, pampu ya dripu, vitanda 6 vya umeme, vitanda mwendo 2, mashine ya mvuke, kipimo cha moyo, mashine ya kupasha joto damu na maji, vyombo 2 vya kuwekea vifaa vya huduma ya dharura, mashine 2 za kunyonya damu wakati wa upasuaji na mashine ya mawimbi sauti.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa