Na. Paul Kasembo, SHY MC.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndugu Godfrey Mnzava amezindua mradi wa maji wa Bugayambelele kata ya Kizumbi unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) ambao utawanufaisha wakazi wa Bugayambelele takribani 10,165.
Mradi huu wa maji umezinduliwa leo tarehe 11 08.2024 na ndugu Mnzava na kuweka jiwe la msingi huku ukigharimu shilingi milioni 150,237,279.
Mnzava ameitaka SHUWASA kuhakikisha inaendeleza mradi huu wa maji wa Bugayambelele na kuhakikisha unawafikia wakazi wengi zaidi.
“Ninawataka muongeze juhudi zaidi ili kuhakikisha mradi huu wa maji wa Bugayambelele unawafikia wakazi wengi ili wao pia wanufaike na mradi huu” amesema Mnzava.
Mradi huu ni moja kati ya miradi 10 ambayo imetembelewa na Mwenge wa Uhuru 2024 kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga yenye thamani ya bilioni 4.2 huku ukikimbia kilomita 74.5.
Jambo kubwa lililomvutia mkimbizaji mwenge kitaifa ni uwepo wa mkakati wa kuongeza mtandao wa bomba za maji km 2.1 zaidi kutoka kwenye kituo hiki cha maji. Ongezeko hili la utoaji huduma litagharimu Tzs. Mil 40 na kwamba fedha hizo zimekwishatengwa kwenye bajeti huku Mkurugenzi wa SHUWASA Eng. Yusuph akiahidi kuanza rasmi utekelezaji huu ifikapo Oktoba 2024.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa