Na. Shinyanga RS.
Mwenge wa Uhuru 2023 umetoa siku 5 kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kituli iliyopo Kata ya Tinde Halmashari ya Wilaya ya Shinyanga kutoa taarifa ya urekebishaji wa kasoro zilizo jitokeza wakati wa ukaguzi ili kuona utekelezaji wa maelekezo hayo.
Maelekezo hayo yametolewa leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndg Abdalla Shaib Kaimu mara baada ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa shuleni hapo huku akisisitiza umakini katika uketekelezaji wa miradi ukizingatia kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano ametoa fedha nyingi katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tinde.
"Niwatake uongozi wa shule ya sekondari Kituli kutoa taarifa ya utekelezaji wa maelekezo tuliyotoa kwenu ili kuona jinsi mlivyotekeleza," alisema Ndg. Kaim.
Pamoja na kazi mbalimbali zilizofanywa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Shinyanga ikiwemo kuzindua, kukagu, kuweka jiwe la msingi pamoja kupanda miti lakini pia umeshiriki kukabidhi vyandarua kwa mama wajawazito, watoto chini ya umri wa miaka 5, wazee katika Kituo cha Afya Tinde pamoja na kuzindua rasmi gari la kubebea wagonjwa la Zahanati ya Mwakitolyo lililotolewa na Wachimbaji Wanawake Wadogowadodo Mwakitolyo Namba 5.
Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga imeangazia miradi 9 ikiwa ni zaidi ya thamani ya Tzs. Bilioni 5.3 na kukimbizwa Kilomita 94.22 ambapo kwa ujumla wake Mwenge umepitisha miradi yote na hakuna uliokataliwa huku akiwapongeza viongozi wote kuanzia Mkuu wa WilayaMhe. Johari Samizi, Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg. Simon Berege na watumishi wote kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo wana Shinyanga DC.
Tarehe 30 Julai, 2023 Mwenge wa Uhuru utakuwa Wilayani Kahama ambapo utakagua, kuzindua na kuona jumla ya miradi 6 yenye thamani ya 3, 697, 546, 277, 80.
@ortamisemi
@christinamndeme18
@shinyangadc_official
@shinyanga_tanzania
Moja kati ya jengo la vyumba vya madarasa katika Sule ya Sekondari Kituli
Upandaji miti ulifanyika pia enro hilo la shule ya Sekondari Kituli
Gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) iliyotolewa na wanawake wachimbaji wa madini Mwak8tolyo namba 5
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa