Na. Paul Kasembo, USHETU.
MWENGE wa Uhuru umeweka Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Machinga iliyopo Nyamilangano katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu huku kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ndg. Eliakim Mnzava akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu Bi. Hadija Kabojela kwa utekelezaji wa mradi huu mzuri wenye lengo la kuwawezesha Machinga kuwa na ofisi yao ukizingatia kuwa hili ni kundi kubwa sana linalojumuisha na bodaboda.
Haya yamesemwa leo tarehe 14 Agosti, 2024 na Mnzava wakati wa ukaguzi na kutembelea jumla ya miradi 7 ya Halmashauri ya Ushetu mradi ambao umegharimu zaidi ya Tzs. 47 ambapo pamoja na mambo mengine lakini pia kulifanyika zoezi la uteketezaji wa madawa ya kulevya aina ga bangi yenye uzito wa Kg. 34 huku ndg. Mnzava akitoa wito kwa wananchi kuwa na malezi mema zaidi kwa vijana wetu kundi ambalo limetajwa kuwa wahanga wakubwa wa madawa ya kjlevya
"Nawapongeza sana Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa mradi huu wa ujenzi wa ofisi ya machinga pamoja na bodaboda, ni mradi mzuri sana wenye tija kubwa ukizingatia kuwa hili kundi kubwa sana amnalo limejiajiri na kupata uungaji mkono mkubwa wa Serikali, hivyo kukamilika kwa ofisi hii kunakwenda kuwaongezea hadhi zaidi," amesema Mnzava.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya Ushetu umekimbizwa kilomita 123, umeifikia miradi ya maendeleo 7 yenye jumla ya zaidi ya Tzs. Bilioni 2.8 huku miradi yote ikipitishwa bila kukwama baada ya Mwenge wa Uhuru kuridhishwa na utekelezaji wake na hivo kuifanya Halmashauri iliyo chini ya Wilaya ya Kahama na ambayo inaongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita na Mkurugenzi wake Bi. Hadija Kabojela kung'ara zaidi.
Miradi iliyofikiwa ni pamoja na Ujenzi wa vyumba vya madarasa 5 Shule ya Msingi Ukune ambapo ilikuwa ni kuzindua, Mradi wa barabara km 1.05 kiwango cha lami na kuwekewa Jiwe la msingi Nyamilangano, ujenzi wa ofisi ya machinga na bodaboda na kuwekewa Jiwe la Msingi Nyamilangano, ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum na kuwekewa jiwe la msningi,mradi wa mazingira, CTC na RUWASA.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa