Na. Shinyanga RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo leo tarehe 14 Oktoba, 2023 amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya mbio za baiskeli zinazoandaliwa na Benki ya CRDB katika uwanja wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na kuwapongeza CRDB lakini pia amesema kuwa mashindano haya yamesaidia kuutangaza mkoa pamoja na kufungua zaidi fursa za kiuchumi kwa wananchi na uwekezaji pia.
Prof. Tumbo amesema haya kwenye kilele cha Mbio hizi za Baiskeli za CRDB Shinyanga (Shinyanga CRDB Cycling Rally) mbele ya washiriki wa mbio hizi na wananchi kuwa, uwepo wa mashindano haya si tu kwamba zinatoa fursa kwa wananchi wanaoshiriki kuimarisha na kulinda afya zao, bali washindi wanapata zawadi zinazowahamasisha wao na wengine kuendelea kushiriki na mashindano mengine zaidi.
“Mbio hizi zimetoa fursa ya kuutangaza mkoa wetu pamoja na kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi na wafanyabiashara. Kadri miaka inavyozidi Kwenda, umaarufu wa mbio hizi unazidi kuongezeka hivyo basi, wakati Benki ya CRDB ikifungua njia, nitumie fursa hii kuziomba pia kampuni nyingine nazo kuangalia namna ya kufungua fursa za mkoa wetu jambo litakalosaidia kuboresha maisha ya wananchi,” alisema Prof. Tumbo.
Awali kulitanguliwa na shughuli za kijamii ikiwemo kuchangia damu ambapo zaidi ya chupa 500 za damu salama zilikusanywa kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wanaotibiwa katika hospitali na vituo vya afya mkoani humu na nchini kote kwa ujumla.
Kwa upande wake Meneja wa CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney akiongea kwa niaba ya Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana amesema mbio hizo hufanyika kila mwaka siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere, ambaye alipenda kila mwananchi kuwa huru kiuchumi kwa kujituma kufanya kazi kulingana na fursa zilizopo kwenye eneo alilopo.
Luther amesema Benki ya CRDB ni mdau mkubwa wa michezo nchini kutokana na imani kubwa kwamba inajenga ushirikiano, mshikamano, na kuwaleta watu pamoja hivyo kuwa rahisi kuleta maendeleo katika jamii.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa