Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewatakia Kila lenye Kheri Timu ya Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) mbao wamechaguliwa kwenda kuwa kuwakilisha Kitaifa mkoani Tabora huku akiwatia moyo na kuwataka karudi na ushindi kwa kushika nafasi ya kwanza.
RC Macha amesema hayo Juni 4, 2024 wakati akifunga Kambi hii ambayo hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga na kuhudhuriwa na Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako pamoja na walimu wa michezo ambapo pamoja na maelekezo mengine amewaahidi wanamichezo hawa kwamba kila timu itakayorudi na Medali itakutana zawadi yake.
Kando na hayo RC Macha ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa kila shule inatenga maeneo ya michezo na kuwawezesha na kuwajengea uwezo wanafunzi wa michezo ili kuwa na vijana wenye uwezo wakati wowote wanapohitajika.
"Nimekuja kuwatia moyo, kuwatakia kila lenye kheri na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu katika ushiriki wenu kwenye UMITASHUMTA Taifa katika Mkoa wa Tabora, nami nawaahidi kwamba kila timu itakayorudi na Medali itakutana na zawaidi nono kutoka kwangu," amesema RC Macha.
Kwa upande wake Bi. Ndalichako amesema kuwa Mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2023 Shinyanga ilishika nafasi ya tatu Kitaifa, kutokana na maandalizi mazuri yaliyofanywa wanao uhakika kuwa watarudi na ushindi kwa kushika nafasi ya kwanza.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Dafroza Ndalichako, akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, ametaja idadi ya wanafunzi ambao wamechaguliwa kuwakilisha UMITASHUMTA Kitaifa Mkoani Tabora kuwa wapo 120 Walimu wa Michezo 15, Mratibu wa Michezo 1 na Daktari 1.
Mashindano haya yamebebwa na Kauli Mbiu “Miaka 50 ya UMITASHUMTA tunajivunia Mafanikio katika Sekta ya Elimu,Michezo na Sanaa, Hima Tanzania shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024”.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa