Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameomba na kuwakumbusha Wajasiriamali wa Sekta ya Ngozi mkoani Shinyanga wanaohudhuria mafunzo yanayoendeshwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuhakikisha wanashirki kikamilifu katika zoezi la kujiandikisha kweye Daftari la Mtaa, Vijiji na Vitongoji kwa ajili ya Kupiga Kura kuanzia tarehe 11 hadi 20, Oktoba 2024 ili waweze kupiga katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba mwaka huu.
Haya ameyasema leo tarehe 9 Septembq, 2024 alipokwa akifungua Mafunzo haya kwa wajasiriamali yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na pongezi kwa kupata nafasi hii ya kushiriki, lakini pia amewataka washiriki kuongeza ubunifu zaidi ili waweze kukua kiuchumi, kibiashara na hatimae kujitangaza Kimataifa kutokea Shinyanga.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba, 2024 utatanguliwa uandikishaji ambapo mpaka sasa maandalizi yote yanakwenda vizuri kama yalivyopangwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa