Na. Paul Kasembo, KAHAMA MC.
MRATIBU wa Uboreshaji Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ndg. Bakari Kasinyo amewaomba wananchi kuangalia namna ya kupunguza foleni na kuokoa muda kwa kutumia bema vituo visinyokuwa na foleni zaidina ambavyo vinapatikana ndi ya mtaa mmojakuweza kupata huduma badala la kubakia kwenye foleni ndefu zaidi kwa sababu tu hicho ndiyo kilichopo karibu yake.
Haya ya,esemwa leo tarehe 25 Agosti, 2024 na ndg. Kasinyo alipotembelea Kituo cha Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura kilichopo Mtaa wa Mhongolo, Kata ya Mhongolo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ambapo kuna watu wengi zaidi wakati kituo cha Shule ya Sekondari Nyashimbi hapakuwa na foleni kabisa ukizingatia vyote hivi vipo ndaninya Mtaa mmoja wa Mhongolo.
"Niwaombe sana Mawakala wote pamoja na hamasa nzuri mnayoitoa na kupata muitikio mkubwa, lakini pia tuwaelemishe wananchi wetu kutumia pia vituo vingine vilivyopo ndani ya mtaa husika kama ambavyo imejionesha katika mtaa huu wa Mhongolo hapa Manispaa ya Kahama ili kuokoa muda na urahisi wa kupata huduma yenyewe," amesema Kasinyo.
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama inatekeleza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumh la Mpiga Kura ulioanza tarehe 21 Agosti, 2027 na utakamilika tarehe 27 Agosti, 2024 ambapo inayo jumla ya vituo 167.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa